Familia ya Raia TV ilijumuika na familia ya mwendazake Edwin Gitau almaarufu kama DJ Big Deal aliyefariki katika ajali ya barabarani mwezi huu.
Marehemu DJ Big Deal alifariki tarehe 9 Juni na kuzikwa juzi Jumatatu kwao Murang’a.
Marehemu alikua mmoja wa kikosi cha kipindi cha Gospel Gumzo kinachopeperushwa hapa Raia TV kila siku ya Jumapili.
